Deuteronomy 23:3-5

3 aHapatakuwa na Mwamoni au Mmoabu au yeyote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi. 4 bKwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimu
Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi.
ili kuwalaani ninyi.
5 dHata hivyo, Bwana Mwenyezi Mungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababu Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapenda.
Copyright information for SwhKC